Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Enrique Mora amesema hayo katika ujumbe aliotuma kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter na kueleza kuwa: Mazungumzo ya Vienna yapo katika hatua nyeti. Tunaelekea kufika tamati baada ya miezi kumi ya majadiliano. Matokeo yake bado hayajulikani.
Mwanadiplomasia huyo wa ngazi ya juu wa EU amebainisha kuwa, bado kuna masuala nyeti yanayotakiwa kupatiwa ufumbuzi, na kwamba wajumbe wa pande zote wanafanya juu chini kuhakikisha kuwa natija inapatikana.
Duru ya nane ya mazungumzo ya Vienna kwa ajili ya kuiondolea Iran vikwazo vya kidhalimu na haramu ilianza tena tarehe 8 mwezi huu wa Februari baada ya mapumziko mafupi kwa lengo la kuchukuliwa maamuzi ya kisiasa.
Iran inasisitiza kuwa inasubiri maamuzi ya Ulaya na Marekani kuhusiana na mazungumzo hayo ya Vienna ya kuondolewa Tehran vikwazo.
342/